MUFTI DKT. SHEKH ZUBER KUONGOZA HARAMBEE YA KUSAIDIA MAHITAJI YA SHULE KWA YATIMA NA UJENZI KITUO CHA COMMUNITY CENTER JIJINI DAR
Mwenyekiti wa asasi ya Volunteer in Development, Bi. Tune Shaabani akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maandalizi ya harambee hiyo, ambapo zaidi ya milioni 82 zinatarajiwa kukusanywa kusaidia Yatima na ujenzi wa kituo cha Community Center jijini Dar es salaam.
Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya harambee hiyo, Bi Zubeda Shomari akizungumza katika mkutano na wanahabari (hawapo pichani) juu ya maandalizi ya harambee hiyo, ambapo zaidi ya milioni 82 zinatarajiwa kukusanywa kusaidia Yatima na ujenzi wa kituo cha Community Center jijini Dar es salaam.
Mratibu wa harambee hiyo Bi. Shaadya Awadh akielezea lengo la harambee hiyo ambapo zaidi ya milioni 82 zinatarajiwa kukusanywa kusaidia Yatima na ujenzi wa kituo cha Community Center jijini Dar es salaam.
Meneja Taasisi ya Volunteers In Development, bwana Kasimu Haruna Bakari akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu malengo ya harambee hiyo, ambapo zaidi ya milioni 82 zinatarajiwa kukusanywa kusaidia Yatima na ujenzi wa kituo cha Community Center jijini Dar es salaam.
Dar es salaam
Taasisi ya Volunteer in Development (VID) inayojishughulisha na kuhudumia yatima, wajane na wanaoishi katika mazingira magumu imeandaa harambee kwa ajili ya kukusanya fedha kwa ajili ya awamu ya kwanza ya ujenzi wa jengo litakalojulikana kama Community Center sambamba na kununua vifaa vya shule kwa yatima zaidi ya 750 jijini Dar es salaam.
Akizungumza jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa asasi hiyo Bi. Tune Shaabani amesema lemgo la harambee hiyo ambayo imelenga kukusanya zaidi ya Million 82 itafanyika tarehe 26 mwezi huu katika hotel Hyatt Regency kilimanjaro ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mufti mkuu wa Tanzania Dkt. Shekh Abubakar Zuberi.
"Ni kawaida kila ifikapo mwanzo wa mwaka taasisi yetu imekuwa ikifanya harambee kwa lengo la kusaidia watoto yatima na waishio ktk mazingira mgumu mahitaji na vifaa mbambalbali vya shule kama sare za shule, viatu, soski, mabegi, madaftari na vifaa vingine vya shule" Alisema Bi.Tune Shaabani
Alisema fedha zitakazopatikana katika harambee hiyo pia zitatumika kuendeleza waitimu waliomaliza kupata mafunzo ya ufundi stadi VETA pamoja na kuwasaidia wahitimu wanaojiunga na elimu juu kuanzia Ngazi ya Astashahada, Stashahada na Shahada.
Aidha bi Shaabani aliongeza kuwa kiasi cha fedha kitakachobakia kitatumika kwa ajili ya awamu ya kwanza ya ujenzi jengo la Community Center ambayo inatarajiwa kuwa kitega uchumi kitakachochangia kipato na kutoa mafunzo ya ufundi stadi kwa wanaoishi katika mazingira magumu kwa lengo la kuwaongezea tija.
Nae mratibu wa harambee hiyo Bi. Shaadya Awadh alisema asasi hiyo ambayo inaudwa na umoja wa wanawake waliokutana katika mtandao wa kijamii wa facebook kwa lengo la kusaidia waliokuwa na mahitaji mbalimbali ya kijamii kama vile matibabu, Ada pamoja na kuchangishana pesa.
"Asasi yetu ni muunganiko wa wanawake walikutana katika mtandao na kusajiliwa rasmi april 26, 2014 kuwa asasi kwa lengo la kusaidia wenye mahitaji pamoja na kuwasaidia kuwapatia mafunzo kuwajengea uwezo hususani kwa wasichana na wanawake" Alisema Bi. Shaadya.
Kwa upande wake Bi Zubeda Shomari alisema tangu kuanzishwa kwa asasi hiyo miaka 12 iliyopita tayali wameweza kutoa msaada kwa yatima na walezi wao wapatao 970 katika mikoa ya Mwanza, Daer es salam, Pwani, Bagamoyo, Tangana visiwa vya Unguja na Pemba.
Mapema Meneja Taasisi ya Volunteers In Development, bwana Kasimu Haruna Bakari amesema jamii inatakuwa kutambua kuwa
jukumu la kusaidia yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ni jukumu la jamii yote
"Nitoe rai kwa jamii itambue kuwa jukumu la kusaidia watu wenye uhitaji hususani yatima na wajane ni jukumu la kila mmoja wetu hivyo asasi ya (VID) kwa kushirikiana wadau na jamii itaendelea kuwasidia walio na uhitaji kwa kutoa fursa za masomo na mafuzo kwa lengo la kuwezesha kujikwamua" alisema bw. Bakari.
Asasi Volunteer in Development ni asasi isiyo ya kiserikali (NGOs) iliyo na usajili namba 00N00071227 kwa lengo la kuwasaidia watoto yatima wanaoishi katika mazingira magumu na wasiojiweza katika jamii kwa lemgo la kuwapa elimu elimu kujikwamua kifikra na kuwapa maarida kujikomboa na umaskini.







