TIGO YAZINDUA KAMPENI MPYA YA "MAGIFTI DABO DABO"
Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Tanzania leo Jumatano Novemba 22, 2023 imezindua kampeni yake mpya ya ‘Magifti Dabo Dabo’ yenye lengo la kusherehekea mafanikio ya wateja wao ndani ya mwaka 2023 unaoenda ukingoni kwa kuwapatia zawadi mbalimbali.
Kampeni hiyo ya siku 80 itahusisha kiasi cha shilingi milioni 30 kutolewa pamoja na magari mawili mapya.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Afisa Mkuu wa TigoPesa Angelica Pesha alisema,
"Nina furaha kubwa kutambulisha kampeni yetu ya 'Magifti Dabo Dabo' ambayo ni kama uthibitisho wa utayari wetu katika kushukuru uaminifu wa wateja wetu. Kampeni hii inadhihirisha hamu yetu ya kuwapatia wateja wetu sio tu bidhaa na huduma za kipekee bali pia kumbukumbu ya kudumu,
Kuhusu Tigo
Tigo Tanzania ni kampuni ya simu ya mtindo wa maisha ya kidigitali inayoongoza Tanzania Kwa zaidi ya miongo miwili ya kuendesha shughuli zake hapa nchini, Tigo imekuwa kiongozi katika uvumbuzi wa kidijitali, ikitoa bidhaa na huduma mbalimbali za sauti, SMS,
intaneti ya kasi ya juu, na huduma za kifedha kupitia simu za mkononi. Tigo ni sehemu ya Axian Telecom Group, watoa huduma za mawasiliano barani Afrika wanaotoa huduma zao katika masoko mengi ya Afrika.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea tigo.co.tz au wasiliana
Woinde Shisael – Meneja Mawasiliano wa Kampuni. Barua Pepe: Woinde.shisael@tigo.co.tz






