Breaking News

CUF YAWATAKA WANANCHI KUTORUDIA MAKOSA KATIKA UCHAGUZI UJAO

Chama cha wananchi (CUF) Kimewataka wananchi kutokufanya makosa katika chaguzi zijazo hususani wa serikali za mitaa hili kuweza kupata viongozi makini watakaoweza kutatua changamoto mbalimbali katika maeneo yao ikiwemo ulinzi na usafi.

Akizungumza katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika katika kata ya buguruni Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa chama hicho, Injinia  Mohamed Ngulangwa amesema wananchi wenyewe ni mashahidi kabla ya kile kilichofanyika mwaka 2019 na kupelekea kupata viongozi wasio wachangua huduma hizo zilikuwa shwali katika kata hiyo.

"Wote hapa ni mashahidi kabla ya uchaguzi wa mwaka 2019 uliopelekea kuingia madarakani viongozi ambao awakuchaguliwa na wananchi hali katika maeneo yote ilikuwa shwali na changamoto zote zilikuwa zikitatuliwa ila mara baada ya uchaguzi huo hali imebadilika kutokana na kushindwa kwao kuwajibika ipasavyo kwa wananchi" Alisema Injinia Ngulangwa.

Alisema zipo taarifa kuwa wapo watu ambao wamekuwa wakipita katika maeneo mbalimbali ya kata hiyo kuwarubuni watu hususani vijana kujiunga na chama cha mapinduzi CCM napenda kutoa rai kwa wananchi na vijana wote kuwa wasikubali kurubuniwa na watu hao kwani yote yanayotokea sasa katika maeneo yao ni matokeo sera mbovu za chama hicho.

Injinia Ngulangwa aliongeza katika kipindi ambacho wananchi wa kata hiyo walichagua viongozi wanaowataka kero zote zilikuwa zikitafutiwa ufumbuzi kwa wakati akitolea mfano swala la usafi na ulinzi katika maeneo hayo kuwa kulikua na utaratibu mahususi kati ya viongozi na wananchi na kuandaa utaratibu mzuri wa kutatua kero hizo.

Akizungumzia juu ya ya mwenendo wa hali ya siasa nchini tangu kuruhusiwa kuanza kwa mikutano ya hadhara amesema bado kuna watendaji wachache hususani jeshi la polisi nchini ambao wamekuwa wakifanya hujuma hususani kwa chama cha wananchi CUF hivyo kukwamisha hazma ya mhe rais ya maridhiano ya kitaifa.

"Kumekuwepo na vitendo vinavyofanywa na jeshi la polisi vya kuhujumu chama cha wananchi CUF vitendo ambacho vimekuwa vikienda kinyume na kauli ya mheshimiwa rais ya kutaka kuwepo na maridhiano ya kitaifa kufatia kutengua zuio haramu lililokuwepo la kuzuia mikutano ya vyama vya siasa nchini"  
Injinia Ngulangwa. 

Alisema vitendo hivyo vya jeshi la polisi vya kuzuia kufanyika kwa mikutano ya chama chetu ambayo ilifata hatua zote za kisheria imekuwa ni hujuma kubwa kwa chama kutokana na jeshi hilo pia kukihuka utaratibu wa kisheria ambao unawataka kutoa taarifa masaa 24 kabla ya kufanyika.

Mkutano huu wa hadhara ambao pia uliudhuliwa na vingozi wa chama hicho mbalimbali unafanyika siku chache baada ya mvutano mkali baina ya CUF- Chama Cha Wananchi na Jeshi la Polisi kufuatia askari Polisi kuvuruga mikutano ya CUF- Chama Cha Wananchi.