Breaking News

DKT. KIKWETE: CHUO CHA MAJI ZALISHENI WATAALAM WATAKAOWEZA KUPAMBANA KATIKA SOKO LA AJIRA

Rais Mataafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akikata Keki katika maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Maji na Kongamano la Tatu la Kimataifa la Kisayansi la maji.

Mkuu wa Chuo cha Maji Dkt. Adam Karia akihutubia katika maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Maji na Kongamano la Tatu la Kimataifa la Kisayansi la maji.

Dar es Salaam
Rais Mstaafu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete  amekitaka chuo cha Maji Dar es Salaam  kuhakikisha kinazalisha Wataalam watakaoweza kupambana katika soko la ajira na kutoa suluhu kwa changamoto zinazoikabili sekta ya maji nchini.

Kauli hiyo Rais Mataafu Dkt.Kikwete ametoa leo Januari 31, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati akifungua maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho na Kongamano la Tatu la Kimataifa la Kisayansi la maji.

Aidha, Dkt. Kikwete   ameutaka uongozi wa chuo hicho cha Maji Dar es Salaam kutumia vema fedha zinatolewa na Serikali ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa katika kumtua Mama ndoo kichwani.

Katika hatua nyingine Rais Mstaafu Dkt. Kikwete amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuishi kauli yake ya kumtua mama ndoo kichwani kwani Serikali imekuwa ikitekeleza miradi mingi ya maji.

Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho Dkt. Adam Karia ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajilj ya chuo hicho ili   kukiwezesha kufanya maboresho mbalimbali.