Breaking News

TANAPA YAVUNJA REKODI YA KUPOKEA WATALII

Katika kipindi Cha mwaka wa fedha 2023/2024 katika kipindi cha kuanzia July 2023 – March 19, 2024 idadi ya Watalii 1,514,726 (wa ndani wakiwa 721,543 na wa nje wakiwa 793,183) wametembelea Hifadhi za Taifa sawa na ongezeko la asilimia 5 ikiwa ni zaidi ya lengo la kupokea Watalii 1,387,987 (wa nje 827,713 na wa ndani 726,676) katika kipindi husika.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es salaam na Kamishna wa Uhifadhi Nchini TANAPA, Nassoro Juma Kuji ambapo amesema idadi ya Watalii wanaotarajiwa kutembelea Hifadhi za Taifa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ni 1,830,081 (Watalii wa nje 963,413 na wa ndani 866,667), pia katika kipindi cha miaka mitatu kumekuwepo na ongezeko la siku za kukaa wageni kutoka wastani wa siku 1,749,194 katika mwaka wa fedha 2021/2022 hadi kufikia wastani wa siku 2,669,586 kufikia February 2024.
Ongezeko hili limechangiwa na juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha shughuli za utalii kupitia Royal Tour