ACT: SERIKALI ITENGE BAJETI YA KUTOSHA KITENGO CHA MAAFA
Serikali imeshauriwa kuendelea kuboresha kitengo cha maafa kwa kutenga bajeti ya kutosha kwa kitengo hicho kiweze kukabiliana na majanga mbalimbali ikiwa pamoja ajali za moto.
Ushauri huo umetokewa jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Kivuli ACT Wazalendo, Isihaka Mchinjita ambapo amesema kuwa mwishoni mwa mwaka 2023 hadi sasa kumekupo na udhaifu mkubwa wa kitengo cha maafa katika kuchukua hatua za dharura pindi majanga yanapotokea.
"Kwa mfano Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) ilitabiri nchi kupokea mvua kubwa lakini watanzania hatukuona hatua madhubuti zikichukuliwa kujiandaa na kujilinda na janga hili ili kuepusha au kupunguza athari zinazowapata wananchi sasa". Alisema bw. Mchinjita.
Alisema ukanda wa Kibiti Rufiji eneo linalozunguka bonde la mto Rujifi hasa liliopo karibu na bwawa la kuzalisha umeme la Mwalim Nyerere kuna hali mbaya sana, ambapo kata zaidi ya 12 zimeripogiwa kuathirika vibaya na maji, mazao, makazi pamoja na huduma msingi za kijamii kuharibiwa vibaya na kuwaacha wananchi wa eneo ilo kwenda kujihifadhi katika majengo ya shule.
Aidha bw. Mchinjita aliongeza kuwa kwa mujibu wa hotuba ya Waziri Mkuu iliyosomwa bungeni haijaonesha hatua za makusudi za kujenga uwezo wa kibajeti kununua vifaa vya kisasa vya uokoaji pamoja na kuijengea uwezo idara ya maafa na taasisi zilizochini yake.
"Act tunaitaka Serikali kuchukua hatua, kutenga bajeti ya kutosha ili kujenga uwezo wa idara ya maafa na kuongeza ufanisi wa usimamizi wa idara hiyo, ikiwemo kutumia teknolojia ya juu ya kufuatilia maafa sehemu mbalimbali za nchi". Alisema bw. Mchinjita.




