TAASISI YA HINATAS FOUNDATION YAANDAA FUTAR KWA KITUO CHA MWANDALIWA ORPHANAGE CENTRAL JIJINI DAR
Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, bwana Ally Bananga akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na taasisi ya Hinatas Foundation kwa watoto yatima na wenye mahitaji maalum wa kituo cha Mwandaliwa Orphanage Center jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hinatas Foundation, Bi. Ayshat Sanya akifafanua jambo katika hafla hiyo ya futari kwa watoto yatima na wenye mahitaji maalum wa kituo cha Mwandaliwa Orphanage Center jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao, Bi Yvonne Cherries maarufu kama (Monalisa) akizungumza katika hafla hiyo ya futari kwa watoto yatima na wenye mahitaji maalum wa kituo cha Mwandaliwa Orphanage Center jijini Dar es Salaam.
Mlezi wa kituo cha Mwandaliwa Orphanage Center ambaye pia ni Afisa, Elimu wa kituo hicho, bwana Omary Daudi akizungumza katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Hinatas Foundation kwa watoto wa kituo hicho jijini Dar es Salaam.
Dar es salaam:
Taasisi ya HINATAS Foundation imefanya hafla maalum ya futari kwa watoto yatima na wenye mahitaji maalum wa kituo cha Mwandaliwa Orphanage Center
Hafla hiyo ambayo imefanyika 6 April 2024 na mgeni rasmi alikuwa, Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, bwana Ally Bananga.
Akizungumza katika ufunguzi wa hafla hiyo bwana Bananga alianza kwa kuipongeza taasisi ya HINATAS Foundation kwa kuandaa hafla hiyo ya futari licha ya kuongozwa na vijana wadogo ila wamefanya makubwa kwa watoto hao kwani ni faraja kubwa kwao.
“Vitabu vya maandiko vya dini zote vinasema Ukimsaidia mtoto yatima au mtu mwenyewe mahitaji maalumu hususani katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa ramadhani ni unaweka hazina nzuri mbele ya Mwenyezi Mungu, ambayo itakusaidia wewe au kizazi chako katika siku zijazo". Alisema bw. Banaga
Alisema jamiii iwe na desturi ya kutoa misaada hasa wa watoto yatima kwani leo hii mzazi wanafurahi kuwa na mtoto au watoto wako wana furaha kuwa na wazazi lakini hutujui yajayo, unaweza kuondoka (kufariki dunia) na kubaki nao yatima.
Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Hinatas Foundation, Bi. Ayshat Sanya akimkaribisha mgeni rasmi amesema hafla hiyo pamoja na kudhamiria kufutarisha watoto 105 pia ililenga kukusanya fedha kwa ajili ya kuwanunulia watoto hao mahitaji mbalimbali ikiwemo nguo na viatu vya kusherehekea sikukuu ya Eid.
"kupitia hafla hii Futari taasisi yetu pia ililenga kukusanya fedha kwa ajili ya kuwanunulia watoto hao mahitaji mbalimbali ikiwemo nguo na viatu ili kuweza kusherehekea sikukuu ya Eid kama watoto wengine". Alisema Bi. Ayshat Sanya
Alisema taasisi hiyo imekuwa ikifanya shughuli zake kwa kishirikiana na wadau kutoka sekta mbalimbali kutekeleza majukumu yake ya kusaidia jamii ameishukuru jamii kwa kuendelea kutushika mkono tangu kuanza, ambapo katika tukio hii la leo tumeweza kukusanya Mil. 3 ambazo zitatumika katika maamdalizi ya watoto hao kuelekea sikukuu ya Eid ikiwemo kununua na kuziwasilisha kituo cha kulewa watoto cha Mwandaliwa Orphanage Center.
Kwa upande wake, Mlezi wa kituo cha Mwandaliwa Orphanage Center ambaye pia ni Afisa, Elimu wa kituo hicho, bwana Omary Daudi ameushukuru uongozi wa Hinatas Foundation na wadau wengine kwa kuwaunga mkono katika kusaidia watoto hao.
‘’Watoto wamefurahi mno kwa futari hii. Lakini tunapoondoka hapa bado tuna mahitaji mengine mbalimbalii kama vyakula, sare za shule sasa tunao usafiri ila changamoto ni hela ya mafuta ya kuweka hivyo tunapenda kuona wadau mbalimbali wakiendelea kujitokeza kuendelea kutusaidia,
kituo cha Mwandaliwa Orphanage Center kina jumla ya watoto 105 kati yao wa kike ni 50 na wa kiume ni 55.










