JENERALI MABEYO AWAVISHA VYEO MAKAMISHNA WAPYA NCAA
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Jenerali Venance Mabeyo (Mstaafu) akimvika cheo Afisa Uhifadhi Mkuu Lilian Magoma ambae amepandishwa kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia idara ya Mipango, tathmini na ufuatiliaji katika tukio lililofanyika 29 Aprili, 2024 Makao makuu ya NCAA Karatu Mkoani Arusha.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Jenerali Venance Mabeyo (Mstaafu) akimvika cheo Afisa Uhifadhi Mwandamizi wa Rasilimali watu, Salma Chisonga aliyepandishwa cheo amevishwa cheo kuwa Kamishna msaidizi Mwandamizi wa uhifadhi, Rasilimali watu na Utawala tukio lililofanyika 29 Aprili, 2024 Makao makuu ya NCAA Karatu Mkoani Arusha.
Karatu - Arusha
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Jenerali Venance Mabeyo (Mstaafu) tarehe 29 Aprili, 2024 amewavisha vyeo maafisa Uhifadhi wakuu waliopandishwa vyeo hivi karibuni katika tukio lililofanyika ofisi za Makao makuu ya NCAA Karatu Mkoani Arusha.
Waliovishwa vyeo ni Afisa Uhifadhi Mkuu Lilian Magoma ambae amepandishwa na kuvishwa cheo kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia idara ya Mipango, tathmini na ufuatiliajI na Afisa Uhifadhi Mwandamizi wa Rasilimali watu Salma Chisonga aliyepandishwa cheo amevishwa cheo kuwa Kamishna msaidizi Mwandamizi wa uhifadhi, Rasilimali watu na Utawala.
Jenerali Mabeyo amewataka makamishna wapya kufanya kazi kwa kujituma na kuzingatia viapo vyao katika misingi ya uzalendo, maadili ya utumishi, ushirikiano, maarifa na bidii ya kazi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.






