Breaking News

PROF. MKENDA KUKUTANA NA WANAUME WA ROMBO WAISHIO JIJINI DAR

Waziri wa Elimu Sayansi na  Teknolojia Profesa Adolf Mkenda ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Rombo mkoa wa Kilimajaro amesema amepanga kukutana na wanaume  wote wa Rombo  wanaoishi katika Mkoa wa Dar es Salaam. 

Mkutano huo ambao utawajumuisha Mbunge wa Rombo, Madiwani na wana Rombo  umepangwa kufanyika Ukumbi wa Kardinali Adams Msimbazi Senta Ilala, agenda ikiwa kujadili maendeleo ya Jimbo la Rombo.

Profesa Mkenda amesema mkutano huo utakaofanyika Mei 5, 2024, si wa kwanza ni mwendelezo wa mikutano aliyofanya Marehemu Bazil Mramba aliyewahi kuwa Mbunge wa Rombo.

Profesa Mkenda amesema Wanaume wa Rombo wamesambaa mataifa mbalimbali wakifanya kazi wanamchango mkubwa kwa wilaya yao wapenda maendeleo na hata maduka mengi ya Kariakoo maneno ya "Chako ni Chako" Dodoma  wengi  hapo ni watu kutoka Rombo.

"Kuhusu kauli zinazosema kuwa wanaume wa Rombo ni walevi wa kutupwa wanaume wa Rombo wamesambaa maeneo mbalimbali na kuna kauli inasema ukienda sehemu usipowakuta Warombo ondoka haraka hivyo wana mchango mkubwa kwa uchumi wa wilaya kama suala ya kunywa wanakunywa baada ya kazi" Amesema Prof. Mkenda

Aidha Prof. Mkenda aliongeza kuwa suala la ulevi Rombo ni jambo linalokuzwa na halina uhalisia kabisa wanaume wa Rombo sio walevi ni wanaume wanaojitambua na wachapakazi.

Akijibu  changamoto ya maji jimboni kwake Profesa Mkenda amesema Wilaya ya Rombo inakabiliwa na shida kubwa ambayo inachangiwa na uhaba wa vyanzo vya maji  hivyo katika mkutano huo wa mei 5, atazungumzia  suluhu  ya tatizo la maji katika Jimbo la Rombo.

Source Jambo blog