ASKOFU MALASUSA MAADILI YAANZIE NA MSINGI
Mkuu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dokta Alex Malasusa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa shule ya msingi na awali ya Jerusalem Mbezi Beach jijini Dar es salaam.
Na Mwandishi wetu - Dar
Mkuu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dokta Alex Malasusa amesema ili tuwe na jamii njema wazazi wametakiwa kutilia mkazo malezi ya watoto wao kimaadili kuanzia ngazi ya msingi ili kusaidia kuondokana na tatizo la mmonyoko wa maadili kwenye jamii.
Ushauri huo ameutoka mapema leo 12 mei 2024 jijini Dar as salaam katika hafla ya uzinduzi wa shule ya msingi na awali ya Jerusalem Mbezi Beach .
"Ili tume na jamii yenye maadili mema ni lazima maadili yajengwe kuanzia ngazi ya awali ya msingi, kwa maadili hayatokei tu" Alisema Askofu Dkt. Malasusa.
Alisema ipo haja ya kuwepo na jitihada za pamoja kati ya wazazi, walezi, walimu na viongozi wa kidini katika kupambana na vyanzo vinavyochochea mmonyoko wa maadili nchini.
"Wazazi na walezi inatakuwa kutambua kuwa Maadili hayatokei tu, au huwezi kwenda kununua maadili ni lazima mimi na wewe tuungane kushirikiana kurudisha maadili mema katika jamii yetu"
Akizungumzia shule kuanzishwa kwa shule hiyo ya Jerusalem, Askofu Malasusa, amesema lengo la kuanzishwa shule hiyo ni kutokana na maadhimio yay mkutano mkuu wa Dayosisi uliketi hivi karibu ambao ulielekeza kuanza kuweka mkazo kwenye elimu, tulianza ngazi ya sekondari sasa tupo kwenye msingi.
Askofu Malasusa amesema shule hiyo ni yakipekee hivyo kutoa wito kwa wazazi na walezi kuwaleta watoto shuleni hapo.
"Shule hii ni ya watu wote, shule hii haina ubaguzi na hatutambagua mtu kwa rangi, dini kila mtu atapata elimu, kwani Yesu hakuja duniani kwa ajili ya watu flani alikuwa kwa watu wote" Alibainisha Askofu Dkt. Malasusa.
Kwa Upande wake Mratibu wa Elimu wa Dayosisi ngazi ya pwani, Bi. Agnes Lema amesema shule hiyo itakuwa ikitumia mtaala wa elimu ya dini kwa ajili ya kuwaleta watoto kwa maadili mema.
Lema alibainisha kuwa lengo la kuanzisha shule hiyo ni baada ya kubaini kuwepo na tatizo kubwa la mmonyoko wa maadili kwenye jamii.
"Tumeona bado kuna changamoto ya kukosa kwa maadili kwa watoto na jamii kwa ujumla, hivyo hapa tutasaidia kumlea mtoto maadili mema" Alisema Bi. Lema.




