SERIKALI IFANYIE KAZI MAPENDEKEZO YA TUME
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini, Dkt. Fredrick Shoo, amesema ameipokea ripoti ya Tume ya Uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa yaliyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 kwa furaha, akieleza kuwa imeliponya Taifa kutokana na majeraha yaliyotokea wakati wa uchaguzi huo kwa kuzungumza ukweli na kutoa mapendekezo muhimu.
Dkt. Shoo amesema iwapo Serikali itayafanyia kazi mapendekezo hayo, Tanzania itaendelea kuwa kisiwa cha amani na mshikamano miongoni mwa wananchi wake,




