GRACE "ZOA ZOA" AWATAKA WANAWAKE KUJIKWAMUA KIUCHUMI
Na Heri Shaaban
Mjumbe wa Baraza la Umoja wanawake (UWT) Wilaya ya Ilala Elizabeth Kilili maarufu kama Mama Zoa zoa amewataka Wanawake Kipawa kujikwamua kiuchumi kwa kubuni biashara zitakazo waingizia mapato.
Mjumbe wa Baraza Elizabeth Kilili, alisema hayo kata ya Kipawa Tawi la Kidarajani wakati wa mkutano mkuu wa Jumuiya ya wanawake UWT ulioandaliwa na Tawi hilo.
"Nawaomba wanawake wenzangu wa Kipawa mjikwamue kiuchumi mzalishe bidhaa bora mkuze mitaji yenu muweze kukuza soko, marufuku pesa za mikopo kuzitumia katika shughuli za sherehe badala yake mkikopa mtumie katika ujasiriamali ". Alisema Dkt. Elizabeth.
Dkt. Elizabeth aliwataka Wanawake mkopo wasinunulie kitu chochote badala yake watumie katika biashara zao walizobuni ili waweze kujiongezea kipato kitakachowakwamua kiuchumi.
Aidha aliwataka wanawake wasichukue mkopo bila elimu ya ujasiriamali ambapo alisema ukichukua mkopo bila elimu uwezi kufanya malengo uliokusudia badala yake unaweza tumia katika shughuli tofauti na malengo yaliokusudiwa.
"Ofisi yangu ipo tayari kutoa elimu bure kwa wanawake inayohusiana na ujasiriamali ili wajikwamue kiuchumi tuweze kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan wanawake tujishughulishe amna kurudi nyuma"alisema .
Aliwataka wanawake wa Wilaya ya Ilala kuwa na upendo na kushirikiana pamoja katika uzalishaji Mali ili malengo yao yaweze kutimia.
Akizungumza na wanawake wa UWT Kidarajani aliwachangia jezi kwa ajili ya mazoezi ya JOGING seti moja wanawake wa UWT ili waendelee kuamasisha Jumuiya ya wanawake ili waongeze Wanachama katika kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa Rais wabunge na madiwani mwaka 2025.




