Breaking News

HAMADI RASHID ANG'ATUKA RASMI UWENYEKITI CHAMA CHA ADC

Mwenyekiti wa chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Mhe. Hamad Rashid Mohamed, ametangaza kustaafu nafasi ya uwenyekiti wa taifa wa chama hicho baada ya kumaliza muda wake kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.

Akizungumza mapema leo makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam Mhe. Hamad Rashid Mohamed amesema anang'uka rasmi kuwa mwenyekiti wa chama hicho nafasi aliokaa kwa kipindi viwili kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.

Amesema tayali amemaliza muda wake mara baada ya kukiongoza chama hicho kwa vipindi viwili.

"Kwa mujibu wa katiba ya chama nafasi ya mwenyekiti wa chama ni awamu mbili za miaka mitano mitano, ambayo inafikia ukingoni rasmi tarehe 27 Juni 2024,". Alisema Mhe. Rashid

Alisema mara baada ya kumaliza uongozi wake chama hicho kitafanya uchaguzi wa mwenyekiti mpya na kutengeneza safu mpya ya uongozi itakayowaongoza katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa vijijini na vitongoji, na hatimaye uchaguzi mkuu wa 2025.

Aidha Mhe Rashid dhamira amewataka na kuwasihi viongozi wa vyama vingine kufuata mfano wa chama chake kwa kuwa na utaratibu wa kuachiana madaraka kwa mujibu wa katiba za vyama vyao.

Katika hatua nyingine Mhe. Rashid amempongeza aliekuwa kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo bwana Zitto Kabwe kwa kuheshimu na kufuata misingi ya katiba katika uongozi wake.