PROF. LIPUMBA KUITIKISA KONDOA KUANZIA MEI 25-29, 2024
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amatarajia kufanya mkutano mkubwa wa hadhara tarehe Mei 26 kondoa ikiwa ni uzinduzi rasmi wa kuanza rasmi kwa mikutano ya hadhara ya chama hicho nchi nzima
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari ilisainiwa na Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma Chama Cha Wananchi CUF, Eng. Mohamed Ngulangwa imesema mara baada ya mkutano huo ambao utadhuliwa viongozi mbalimbali waandamizi 26 mei na kufatiwa Kikao cha siku mbili cha wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa BKUT, Mei 27 na 28.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa Kikao cha BKUT kinatarajiwa, pamoja na mambo mengine, kupitisha majina ya wagombea nafasi za Uenyekiti wa Wilaya na Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa (kuwakilisha wilaya) kwenye Uchaguzi wa Wilaya unaotarajiwa kufanyika mara baada ya Kikao hicho cha BKUT kote nchini.
THE CIVIC UNITED FRONT(CUF- Chama Cha Wananchi)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:
CUF - Chama Cha Wananchi kimepanga kuivuruga Tanzania nzima kwa mfululizo wa matukio ya mikutano mikubwa ya hadhara na harakati za Uenezi zitakazoambatana na mapokezi ya mamia ya wanachama wapya kutoka vyama mbalimbali na wasio wanachama wa chama chochote.
Baina ya Mei 25 na 29 CUF- Chama Cha Wananchi kitawasha moto mkali Wilayani Kondoa ambao kwa hakika utatikisa Tanzania. Mkutano Mkubwa wa Hadhara utakaohutubiwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa Prof. Ibrahim Lipumba na viongozi wengine waandamizi unatarajiwa kufanyika Mei 26 na kufuatiwa na Kikao cha siku mbili cha wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa (BKUT), Mei 27 na 28. Kikao cha BKUT kinatarajiwa, pamoja na mambo mengine, kupitisha majina ya wagombea nafasi za Uenyekiti wa Wilaya na Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa (kuwakilisha wilaya) kwenye Uchaguzi wa Wilaya unaotarajiwa kufanyika mara baada ya Kikao hicho cha BKUT kote nchini.
Moto utakaowashwa Kondoa utaenezwa nchi nzima kwa matukio ya mikutano ya hadhara na harakati zingine za Uenezi kuelekea Uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji mwaka huu na Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge, wawakilishi na madiwani mwakani. Usikose kufuatilia nini kinaenda kutokea Kondoa.
HAKI SAWA NA FURAHA KWA WOTE!
Eng. Mohamed Ngulangwa
Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma
CUF- Chama Cha Wananchi
Mei 13, 2024




