Breaking News

SIKU YA AFRIKA KUFANYIKA MEI 18

Maadhimisho ya siku ya Afrika mwaka 2024 ambayo kwa Tanzania yanatarajiwa kuanza kufanyika tarehe 18 Mei kwa matukio Mbalimbali ikiwemo mbio za Marathon (Africa Day Marathon) ikiwa ni kujumuika na kudumisha umoja wa Afrika.

Akizungumza juu ya maandalizi ya maadhimisho hayo jijini Dar es salam wakati akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Balozi Ally Bujiku amesema maandalizi yote kuelekea siku hiyo yamekamilika na kwa kutambua kuwa michezo ni afya na michezo huleta watu pamoja na michezo hufanya watu wakishirikiana na kuwa na furaha na hiyo itakuwa ni maalumu kwani ni kuazimisha wiki ya Afrika.

"Kwa kutambua kuwa michezo ni afya, michezo huleta watu pamoja na michezo hufanya watu wakishirikiana na kuwa na furaha hivyo tumeamua kutumia michezo kama fursa katika kuazimisha wiki ya Afrika" Alisema Balozi Bujiku.

Alisema pia kutakuwa na siku maalumu ya Dinner Galar ambapo kila Taifa litawasilisha chakula chake cha asili hivyo kutoa fursa kwa Waafrika wote kuchangamana na kubadilishana uzoefu hususani katika mambo ya kitamaduni. 

Aidha BaloI Bujiku aliongeza kuwa maadhimisho ya mwaka huu sambamba na kuwepo kwa mtirirko wa matukio pia kutakuwa na Changizo kwa shule nne za wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika lengo likiwa ni kuboresha mazingira ya elimu ambayo ndio msingi wa Maendeleo ya Taifa.

Akizungumza kwa niaba ya mabalozi walioshiriki mkutano huo Balozi wa Morocco nchini ambaye pia ni katibu wa mabalozi amesema kupitia Marathon hiyo ambayo itakuwa na Km 15 tutashiriki kwa kukimbia na kuimba na kuamasisha kuwa wamoja kwa kuzielekeza dhamira zetu kutatua changamoto zetu.

Awali mkuu wa kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga
akizungumzia namba maadhimisho ya mwaka huu yatakavyokuwa amesema washiriki mbio za kilometa 5 na kilometa 15 watachangia Tsh 30,000/= kila mmoja kwa ajili ya kupata vifaa vya ushiriki.

“Kilele cha maadhimisho ya siku ya mwafika mwaka huu kilipaswa kusherehekewa Mei 25 lakini kutokana na Tanzania kuwa Mwenyeji wa mkutano wa Kimataifa wa Baraza Amani na usalama siku hiyo hiyo tukaona tusherehekee kabla”. Alisema Balozi Kasiga.