TFS NA KAMPUNI TYLLIUM WAINGIA MAKUBALIANO KUDHIBITI MAJANGA YA MOTO MSITUNI
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania na Kampuni ya Tyllium ya Ufaransa, leo wamesaini makubaliano (MoU) kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mradi wa kuimarisha bionuwai ya misitu kwa kudhibiti moto wa msituni na kuimarisha ufugaji nyuki.
Makubaliano hayo yamesainiwa leo tarehe 27 Mei 2024 na Prof. Dos Santos Silayo kwa upande wa TFS na Bw. Bruno Schambacher kwa upande wa Tyllium. Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo imefanyika sambamba na kongamano la biashara kati ya Tanzania na Ufaransa linaloendelea katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.





