TUJIKITE KUANGALIA FURSA NA KUONDOA CHANGAMOTO.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Bi. Agness Meena amewataka wadau wa Bonde la ziwa Victoria kuangalia fursa ili kunufaisha jamii, pamoja na kuondosha changamoto zilizopo.
Amesema hayo jijini Dar es salaam akifungua mkutano wa ngazi ya juu wa kisekta kuhusu uwekezaji wa muda mrefu, mafanikio na changamoto katika bonde la ziwa Victoria.
“Jukumu kubwa sio kukabiliakana na changamoto peke yake, ila kutumia fursa zilizopo ili kuinufaisha jamii inayohudumiwa”. Alisema Mhe Meena.
Pamoja na wengine , kikao hicho kilichoandaliwa na Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria kimewakutanisha wajumbe kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki , Kamisheni ya Bonde la ziwa Victoria, Chama cha Wavuvi wa Ziwa Victoria, Benki ya Dunia na wadau wa maendeleo




