Breaking News

CGF MASUNGA ATEMBELEA HOSPITALI YA MLOGANZILA

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) John Masunga (wa kwanza kulia mwenye suti) tarehe 10 Juni 2024 ametembelea Hospitali ya Muhimbili - Mloganzila na kupokelewa na mwenyeji wake Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Prof. Mohamed Janabi ambapo walijadili ushirikiano kati ya Jeshi na Hospitali hiyo kwa kuunda timu kutoka Zimamoto na Muhimbili ili kuwezesha ushirikiano huo.

Aidha, akiwa hospitalini hapo, CGF Masunga alimjulia hali Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Koplo Hamisi Kungwi aliyepata ajali ya kuungua na moto akiwa katika majukumu ya kuzima moto