Breaking News

JESHI LA ZIMAMOTO LASHIRIKI UZINDUZI WA CHUMBA CHA KUFUATILIA MWENENDO WA MAJANGA

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji likiongozwa na Naibu Kamishna (DCF) Goodluck Urio Zelote na Maafisa Wengine limeshiriki hafla ya Uzinduzi wa Chumba cha Kufuatilia Mwenendo wa Majanga (Stuation room for Multi-Hazard Monitoring and early Warning) pamoja na kurasimisha mfumo wa jukwaa la kielektroniki la myDEWETRA. Hafla hiyo imefanyika leo Juni 14, 2024 Jijini Dodoma
 
Hafla ya Uzinduzi wa chumba hicho imeandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) ikiongozwa na Waziri Mwenye dhamana Mhe. Jenista Mhagama kwa kushirikiana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupunguza Madhara ya Maafa katika kanda ya Afrika na Taasisi ya CIMA Research Foundation ya Nchini Italia.

Chumba hicho na mfumo wa myDEWETRA kitatumia taarifa za Kijiografia kwa ajili ya Uchambuzi wa utabiri wa hali ya hewa na haidrolojia hatarishi ya mafuriko ya ukame, na kutoa tahadhari ya awali kwa wakati na eneo husika, hivyo kuwezesha kuchukua hatua mapema ili kuzuia au kupunguza madhara, kujiandaa na kukabiliana na Maafa.