Breaking News

DOYO ARUDISHA FOMU KUGOMBEA NAFASI YA UENYEKITI WA CHAMA CHA ADC TAIFA

Mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa chama cha Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) Bwana Doya Hassan Doyo leo Juni 19, 2024 amerudhisha famu makao makuu ya chama hicho buguruni jijini Dar es salaam. 

Akizungumza mara baada ya kuoikea fomu katibu wa kamati ya uchaguz bwana Innocent Siriwa amesema amepokea fomu hiyo na kuikagua imekidhi vigezo vyote vinavyotakiwa na chama kuwa mgombea wa nafasi hiyo ya juu ya chama.

"Leo nimepokea fomu ya mtia nia wa kugombea nafasi ya uenyekiti wa vhama chetu. Na kwa mujibu wa katiba na sera za chama fomu hiyo imekidhi vigezo vilivyoainishwa kugombea nafasi hiyo" Alisema Bw. Siriwa.

Alisema zoezi la kupkea fomu kutoka wanachama waliochukua fomu kugombea nafasi Mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho bado linaendelea mchi nzima.

Aidha katika hatua nyingine bwana Siriwa ametoa rai kwa wagombea kufuata taratibu za uchaguzi wakati wa kampeni lakin pia kufuata kanuni na taratibu za chama wakati wa kampeni, alikadhalika amewataka kufanya kampeni za amani na zisilete mgawanyiko wa chama.

Uchaguzi wa chama hicho unatarajiwa kufanyika Juni 29, 2024 ambapo wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho wapigiwa kura ikiwemo nafasi ya mwenyekiti wa chama ambayo inagombewa na bwana Doyo Hassan Doyo kufatia aliekuwa mwenyekiti wa chama hicho mhe. Hamad Rashid kumaliza mda wake kwa mujibu wa sheria za chama.