MR MANGURUE AMTAKA MSEMAJI WA YANGA ALLY KAMWE
Na Neema Mpaka - Dar
Mfanyabiashara maarufu bwana Saimoni Mkondya "Mr Manguruwe" ameweka wazi nia yake ya kumtaka Msemaji wa Yanga Ally Kamwe kuwa msemaji wake binafsi na shughuli zake mbalimbali anazozifanya hususani biashara.
Akizingumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Saimoni Mkondya maarufu kama "Mr Manguruwe" amesema yupo tayari kuuvunja mkata wa Ally Kamwe na Yanga kwa gharama yoyote ile timu hiyo itakatoiitaji kwani amemnadi msemaji huyo kwa kusema kuwa Ni mtu anayejua kazi yake.
Pia amemuahidi Msemaji huyo kuwa endapo atakubali ofa yake ya kuwa msemaji wake binafsi na nitamlipa mshara mnono yani mara mbili ya anaoupata sasa.
"Nimwambie kuwa kama atakuwa tayali kuja kufanya kazi na mie nitamlipa mshahara mnono ikiwa ni pamoja na kumwongezea malupulupu mengine kuliko alipokuwa anafanya lemgo ni kunwezesha kutulia na kufanya kaz yake kwa ufanisi zaidi" Alisema Mr Mangurue.




