RIDHWANI ATETA NA VIONGOZI CHALINZE
Waziri Ridhwani Kikwete alitoa nasaha zake kwa madiwani na watendaji wa Halmashauri ya Chalinze kuhusu utekelezaji wa dira ya maendeleo ya mwaka 2050. (Picha na Rajabu Shariffu)
Na mwandishi wetu - Mbunge wa Chalinze ambaye ni Waziri wa Nchi ofisi ya Rais menejimenti utumishi na utawala bora mh Ridhwani Kikwete amewataka watendaji na madiwani wa Halmashauri hiyo kushirikiana katika kutekeleza mpango wa Taifa wa maendeleo ya dira 2050.
Katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Chalinze. Mkoa wa Pwani Ridhwani amewahimiza kushirikiana ili kila mmoja atimize wajibu wake kwa uzalendo, maarifa na uadilifu.
Naso viongozi waandamizi wakisemo maafisa Tarafa, wakuu wa idara na madiwani walieleza kuzingatia ushirikiano zaidi chini ya uongozi wa Mkurugenzi wa hamashauri Bwana Ramadhan Possy.
Kwa kauli mbiu ya Rais Samia Suluhu Hassan ya Kazi na utu, tunasonga mbele walimtaka mbunge wao huyo aendeles kufuatilia utekelezaki wa miradi iliyopo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa ngazi zote.




