RAIS DKT. MWINYI KUSHIRIKI UZINDUZI WA SGR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi atashiriki Uzinduzi wa Usafiri wa Treni ya Umeme kwa kutumia Reli ya Kisasa (SGR).
Uzinduzi wa mradi wa SGR utafanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusafiri na treni hiyo safari yenye umbali wa kilomita zaidi ya 400 ambayo inatarajiwa kuanza jijini Dar es Salaam tarehe: 01 Agosti 2024.
Vilevile Rais Dk. Mwinyi atashiriki uzinduzi huo kwa kupanda treni hiyo kuelekea Dodoma.




