Breaking News

DKT. SAMIA: TUTAENDELEA KUCHUKUA HATUA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA DAKTARI NCHINI.

Rais Dokta Samia Suluhu Hassan akizungumza katika kilele cha kongamano ya kumbukizi ya tatu ya Rais Mstaafu wa awamu ya tatu hayati Benjamini Mkapa ambapo kongamano hilo lililoratibiwa na Taasisi ya Benjamini Mkapa (BMF). katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Julai, 2024.
Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambaye pia ni Msarifu wa Taasisi ya Benjamin Mkapa akiongea katika kilele cha kongamano ya kumbukizi ya tatu ya Rais Mstaafu wa awamu ya tatu hayati Benjamini Mkapa ambapo kongamano hilo lililoratibiwa na Taasisi ya Benjamini Mkapa (BMF). katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Julai, 2024.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akifafanua jambo Katika kilele cha kongamano ya kumbukizi ya tatu ya Rais Mstaafu wa awamu ya tatu hayati Benjamini Mkapa ambapo kongamano hilo lililoratibiwa na Taasisi ya Benjamini Mkapa (BMF). katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Julai, 2024.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo (BMF), Dkt Hellen Senkoro akifafanua jambo Katika kilele cha kongamano ya kumbukizi ya tatu ya Rais Mstaafu wa awamu ya tatu hayati Benjamini Mkapa ambapo kongamano hilo lililoratibiwa na Taasisi ya Benjamini Mkapa (BMF). katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Julai, 2024.

Dar es salaam:
Serikali imesema itaendelea kuchukua hatua mbalimbali kukabiliana na upungufu wa Madaktari kwani kadri nchi inavyopiga hatua kwenye maendeleo ndivyo uhitaji wa watumishi katika sekta ya afya unavyozidi kuongezeka.

Akizungumza katika kilele cha kongamano ya kumbukizi ya tatu ya Rais Mstaafu wa awamu ya tatu hayati Benjamini Mkapa ambapo kongamano hilo lililoratibiwa na Taasisi ya Benjamini Mkapa (BMF). Rais Dokta Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inafahamu umuhimu wa sekta hiyo na inatambua upungufu uliopo.hivyo ametoa rai kwa wizara zote ambazo zinahusika na uajili pindi wanapotoa ajira katika sekta waajiri na madaktari wa mkataba ili waweze kujitolea katika hospitali na vituo vya afya vilivyopo nchini.

"Hapa nataka kuwa shahidi juu ya upungufu huo ninapozunguka mikoani na wilayani changamoto namba moja ninayokutana nayo ni upungufu wa watumishi katika sekta ya afya na elimu na hii inatokana na ongezeko la watu na tunaendelea kuzaliana kila siku kwa hiyo mahitaji ni makubwa na ndio maana kila tunavyoajiri watumishi bado wanakuwa hawatoshi". Alisema Dkt. Samia.

Alisema upatikanaji ajira hizo utaendana na ukuaji wa uchumi na ndio maana zinapopatikana nafasi ndogo uchumi ukiongezeka na watumishi sekta ya afya na elimu kunakuwa na upungufu.

"Tumekuwa kukizalisha Madaktari na wataalam wengi kila.mwaka katika vyuo vyetu na hatuwapi ajira lazima tuangalie namna ya kutatua changamoto hii". Alisema Rais Samia

Kwa upande wake Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema miongoni mwa mambo yaliyoibuka kwenye kongamano hilo pamoja na uzalishaji wa madaktari, Wauguzi, wafamasia, wataalamu wa maabara lakini kukosekana kwa ajira kwa wataalam waliopo.

Alisema miongoni mwa maazimio yaliyofikiwa ni pamoja na kuhakikisha hospitali zinaajili watumishi wa mikataba ambapo mchakato wa bima ya afya kwa wote utakapokamilika utaziwezesha hospitali nchini kuajiri watumishi wa mikataba.

Waziri Ummy aliongeza kuwa serikali itakaa na mabaraza ya wanataaluma wakiwemo MAT, wafamasia, wauguzi, maabara ili wakubaliane namna bora ya kudhibiti watumishi wa afya ambao wapo barabarani.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo (BMF), Dkt Hellen Senkoro akizungumza katika kongamano hilo amesema katika kipindi cha miaka 18 tangu kuanza kwa taasisi hiyo imeweza kutoa jumla ya ajira 13,000 katika sekta ya afya ambapo zinajumuisha wataalam 7000 wanaojulikana kama Mkapa Fellows na wahudumu ya afya ngazi ngazi ya jamii 6,000.

Ameongeza kuwa pia Taasisi hiyo imetoa ufadhiri wa masomo kwa wanafunzi 1,150 ambao walikwenda vyuoni na kuhitimu katika fani mbalimbali za afya na wengine wanaojiendeleza wakiwa kazini.

Picha mbalimbali za matukio katika kilele cha kongamano ya kumbukizi ya tatu ya Rais Mstaafu wa awamu ya tatu hayati Benjamini Mkapa ambapo kongamano hilo lililoratibiwa na Taasisi ya Benjamini Mkapa (BMF). katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Julai, 2024.