MADAKTARI BINGWA HOSPITALI YA TEMEKE WATOA HUDUMA KATIKA KAMBI YA MDAKTARI BINGWA KANDA YA KUSINI MASHARIKI LIGULA – MTWARA
Baadhi ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Temeke wakiendelea kutoa huduma kwa wananchi wa Mtwara waliojitokeza katika kambi rasmi ya matibabu ya mdaktari bingwa wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kanda ya kusini mashariki inayofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mtwara – Ligula
Miongoni mwa madaktari bingwa waliotoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Temeke ni Pamoja na mabingwa wa magonjwa ya ndani, daktari bingwa wa macho, meno, daktari bingwa wa magonjwa ya Masikio, Pua na Koo, Daktari bingwa wa Magonjwa ya akili, daktari bingwa wa magonjwa Ngozi, magonjwa ya Watoto, magonjwa ya wanawake na uzazi, mtalaamu wa viungo na utengamao na wengine wengi
Kambi hii rasmi ya matibabu ya kibingwa ni fursa muhimu ya wananchi wa Mtwara na maeneo ya Jirani kupata huduma za kibingwa kwa gharama nafuu, kambi ilianza rasmi tangu tarehe 5 mei, 2025 na itahitishwa tarehe 9 Mei, 2025 wananchi wote mnakaribishwa.








