MHE. CHAKWERA AWASILI TANZANIA KWA ZIARA YA KIKAZI
Mhe. Lazarus Chakwera, Rais wa Zamani wa Jamhuri ya Malawi na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mhe. Shirley Ayorkor Botchwey, amewasili nchini tarehe 08 Aprili 2026 usiku kwa ziara ya kikazi. Mhe. Chakwera amepokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe.





