Breaking News

NIDA YAMNASA KINARA WA KUTENGENEZA VITAMBULISHO FEKI

Dar es salaam - Mamlaka ya Vitambulisho Vya Taifa (NIDA) imefanikiwa kumkamata Danford Mathias Mkazi wa Chalinze Mkoani Pwani ambaye alikuwa anajihusisha na utengenezaji vitambulisho feki kwa Wananchi 

Akizungumza mapema leo Mei,2,2025 Jijini Dar es salaam, msemaji wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) bwana Geofrey Tengeneza amesema imefanikiwa kumkatama mtuhumiwa mmoja kwa kosa kujiihusisha na utengenezaji wa vitambulisho feki vya taifa kwa wananchi wenye namba za utambulisho NIN.

Bwana Tengeneza alisema katika kipindi cha miezi kadhaa sasa kumekuwepo na wimbi kubwa la watu na kuwatapeli wananchi kwa kujinadi kuwa wanaweza kuwapatia wananchi huduma zitolewazo na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Amesema kuwa  baada ya wimbi hilo NIDA iliamua kufanya operesheni maalumu ambapo tarehe April 23, 2025 saa 9.00 alasiri kwa wakishirikiana na Jeshi la Polisi tulifanikiwa kumkamata mtuhumiwa Danford Mathias ambaye ni kinara wa kutengeneza vitambulisho feki vya Taifa.

“Mtu huyo aliyekuwa akijihusisha na utengenezaji na uchapishaji wa Vitambulisho vya Taifa bandia,mpaka sasa bado anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi na hivi karibuni atafikishwa Mahakamani”. Alisema Bw. Tengeneza.

Alisema kukamatwa mtuhumiwa huyo  ni kufatia kupata taarifa kutoka kwa wasamalia wema kuwa anajihusisha na vitendo hivyo ambapo tuliweka mtego na kufanikisha kumkamata pamoja na vifaa vyake.

“Mtuhumiwa alikuwa akitengenezea wateja, vitambulisho feki katika steshenari yake iitwayo Bwanga studio iliyopo Msata Chalinze kwa malipo kati ya Tsh. 6,000/- па 10.000”. alisema.na kuongeza kuwa

"katika mchakato wa utengenezaji wa vitambulisho feki, Mathias hutumia kitambulisho chake halali cha NIDA na kuki-scan na kisha kukiingiza kwenye mfumo wa ADOBE na kufuta taarifa zake, na kubandika taarifa za mteja”. Aliongeza Bw. Tengeneza

Amesema imebainika kuwa katika utengenezaji na uchapishaji wa Vitambulisho feki, baadhi ya watu wanaojishughulisha na biashara hiyo ni pamoja na wamiliki wa maduka ya steshenari.

"Wafanyabiashara hao mbali na kujishughulisha na huduma ya steshenari kama ilivyo katika leseni zao wamekuwa wakijihusisha na utengenezaji na uchapishaji vitambulisho vya Taifa feki kwa wananchi wenye Namba za Utambulisho wa Taifa (NIN) kwa malipo ya fedha". Alisema Bw. Tengeneza.

Halikadhalika ameongeza kuwa kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo,kwa sasa maofisa wa NIDA wameanzisha operesheni maalum nchi nzima  ya kuwasaka na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wale wote wanaojihusisha na utapeli huo.

Bw. Tengeneza ametoa wito  kwa wamiliki wote wa maduka ya steshenari kutojihusisha kwa namna yoyote ile na utengenezaji au uchapishaji wa vitambulisho feki vya Taifa kwani kufanya hivyo,ni kosa la jinai hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaobainika.

Katika hatua nyingine mamalaka ya vitambulisho vy taifa NIDA imetangaza rasmi kuzifungia namba ambazo wahusika wametumiwa ujumbe wa wito wakuchukua vitambulisho vyao hawakwenda.

'Tumeziondoa rasmi namba hizo katika mfumo ila ifahike kuwa unapofungwa namba haina maana kwamba ndiyo basi utambulisho wako umefutwa hapana, unatakiwa kwenda kuchukua Kitambulisho chako Namba yako inarudishwa (activated) na kuanza kutumika tena". Alisema Bw. Tengeneza