RAIS SAMIA AMKARIBISHA RAIS NETUMBO NANDI-NDAITWAH IKULU DAR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amempokea Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mheshimiwa Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah, leo Mei 20, 2025, katika viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Ziara hiyo ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kiuchumi kati ya Tanzania na Namibia, ambapo viongozi hao wanatarajiwa kufanya mazungumzo rasmi kuhusu masuala ya maendeleo, biashara, uwekezaji, na ushirikiano katika sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi.
Mapokezi hayo yamefanyika kwa heshima zote za kitaifa, ikiwemo gwaride rasmi na nyimbo za mataifa yote mawili kupigwa. Mazungumzo kati ya viongozi hao pia yanatarajiwa kuimarisha mahusiano ya kihistoria kati ya nchi hizo mbili.











