WAZIRI MAVUNDE MGENI RASMI UZINDUZI WA KAMATI YA TAMISA JIJINI DAR
Mwenyekiti wa Kamati ya TAMISA, Masoko na Mawasiliano, Dk. Sebastian Ndege akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi rasmi Kamati ya Chama cha Wasambazaji wa Sekta ya Madini Tanzania (TAMISA) jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti TAMISA Bwana Peter Kumalilwa akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya uzinduzi rasmi Kamati ya Chama cha Wasambazaji wa Sekta ya Madini Tanzania (TAMISA) jijini Dar es salaam.
Dar es salaam - Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde anatarajiwa kuzindua kuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Kamati ya Chama cha Wasambazaji wa Sekta ya Madini Tanzania (TAMISA), uzinduzi ambao utaenda sambamba na Kongamano la Kubwa litakalo wakutanisha Watanzania waliopo katika sekta ya madini.
Akizungumza mapema leo Mei 14, 2025 Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya TAMISA, Masoko na Mawasiliano, Dk. Sebastian Ndege amesema siku ya uzinduzi ambao utafanyika Mei 16, 2025 kutakuwa na matukio mawili, mosi ni kuzinduzi rasmi wa Kamati ya TAMISA na kufatiwa na Kongamano litakalowaleta pamoja wadau wa sekta hiyo kujadiliana na kubadilishana uzoefu juu ya nafasi na mchango ya Watanzania katika utoaji huduma kwenye sekta ya madini.
“Tunafahamu sisi Watanzania madini ni ya kwetu, na tunafahamu ya kuwa tunakila sababu ya kushiriki katika uchumi wa madini na Serikali yetu pamoja na Waziri wetu Mhe. Mavunde amekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha kuwa wanaweka mazingira rafiki zaidi hili kuobgeza ushiriki wa Watanzania katika sekta hii,”. Alisema Dkt. Ndege.
Kwa upande wake Mwenyekiti TAMISA Bwana Peter Kumalilwa amesema serikali imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa sekta hiyo inawanufaisha pia wazawa kwani katika sekta hiyo kuna kiasi cha shilingi trilioni 3.1 ambayo inatumika kila mwaka katika manunuzi ambayo angependa Watanzania wanufaike nayo.
“Tayali Kuna migodi mikubwa mitano nchini, ambayo kila mwaka inafanya manunuzi ya shilingi trilioni 3.1, sisi Watanzania tunanufaika kwa asilimia 10 tu, kiasi hiki ambacho ni kidogo sana,”. Alisema Bw. Kumalilwa na kuongexa kuwa
"Kwa kutambua hilo TAMISA imeanza kuchukua hatua kwa kuandaa mkakati ya kuhakikisha Watanzania zaidi wanaanzisha viwanda vya madini na kushiriki kikamilifu katika sekta hiyo ili kuweza kunufaika japo na asilimia 30 ya kiasi cha hicho shilingi trilioni 3.1 za manunuzi ya sekta ya madini"
Aidha Bw. Kumalilwa
aliongeza kuwa sisi kama wazawa tuna sheria ya local content hivyo TAMISA itahakikisha kuwa wazaw pia wananufaika na shilingi trilioni 3.1 za manunuzi japo kwa asilimia 20 hadi 30,
“Mara nyingi tumekuwa tukilalamika kuhusu wageni wanaokuja nchini na kuchukua kazi zetu, sasa sisi kama TAMISA l tutakihakikisha tunawajengea uwezo wazawa ili waweze kushiriki katika uchumi wa sekta ya madini nchini,”. Alisema Bw. Kumalilwa.






