KANYASU AOMBA TENA RIDHAA YA KUONGOZA GEITA MJINI
Mbunge wa Geita Mjini anayemaliza muda wake, Mheshimiwa Costantine John Kanyasu, ameomba tena ridhaa ya wananchi kwa kuchukua fomu ya kugombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), akilenga kuendelea kulitumikia jimbo hilo kwa muhula mwingine.
Kanyasu, ambaye amehudumu tangu mwaka 2015, amesema anaingia tena katika kinyang’anyiro hicho kwa ujasiri na matumaini makubwa, akisisitiza kuwa ametekeleza kwa mafanikio makubwa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 hadi 2025 kwa kiwango cha asilimia 100.
Mbali na kuwa Mbunge, Kanyasu amewahi pia kuhudumu kama Mkuu wa Wilaya ya Ngara na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, nafasi zilizompatia uzoefu wa kiuongozi alioutumia katika kuwatumikia wananchi wa Geita Mjini.
Ameeleza kuwa mafanikio yaliyopatikana katika kipindi chake cha uongozi ni pamoja na uboreshaji wa huduma za kijamii, miundombinu, elimu na afya, na kwamba bado ana maono mapana ya kuendeleza maendeleo hayo endapo atapewa ridhaa tena na wananchi.





