Breaking News

WILLIAM NGELEJA ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SENGEREMA KUPITIA CCM

SENGEREMA – Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Sengerema kuanzia mwaka 2005 hadi 2020, William Mganga Ngeleja, ametia nia ya kurejea bungeni baada ya kuchukua fomu ya kuwania ubunge wa jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Ngeleja, ambaye pia aliwahi kushika wadhifa wa Waziri wa Nishati na Madini, alipokelewa kwa shangwe na mamia ya wananchi mara baada ya kurejea kutoka kuchukua fomu hiyo. Wananchi walifunga barabara wakimlazimisha kusimama na kushuka kutoka kwenye gari lake ili kusalimiana nao, wakieleza kuwa bado wanathamini nidhamu na uwajibikaji wake wakati alipokuwa mbunge wao.

Kitendo hicho kilidhihirisha namna ambavyo wananchi wa Sengerema bado wanamkumbuka na kumheshimu kutokana na mchango wake katika maendeleo ya jimbo hilo.

Ngeleja anatarajiwa kushindania nafasi hiyo katika mchakato wa kura za maoni ndani ya chama hicho tawala.