MADAKTARI BINGWA WA RAIS SAMIA SASA WAPO DAR
Dar es salaam - Wakazi wa jiji la Dar es Salaam na maeneo ya jirani wametakiwa kujitokeza kwa wingi Kuanzia Juni 9 hadi Juni 14, 2025 kupata huduma za matibabu ya kibingwa kutoka kwa Madaktari Bingwa 35 wa Rais Samia.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Edward Mpogolo akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewahimiza wananchi kuchangamkia fursa hii.
"Nawaomba wananchi wenye shida mbalimbali za kiafya kutumia nafasi hii adimu kufika katika hospitali zilizo karibu nao ili kupata huduma za kibingwa kwa gharama nafuu," alisema Mpogolo.
Alisema Madaktari hawa bingwa watatoa huduma katika hospitali tano za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambazo ni Hospitali ya Kivule, Hospitali ya Kigamboni, Hospitali ya Mwabepande Hospitali ya Mbagala Rangitatu, Hospitali ya Ubungo Kimara
Dc Mpogolo amebainisha kuwa zoezi hilo litaenda sambamba na Kujenga Uwezo wa Wataalamu wetu mbali na kutoa huduma kwa wananchi, ujio wa madaktari hawa pia unalenga kuwajengea uwezo na kuwapa elimu na ujuzi madaktari wengine waliopo katika Halmashauri za Mkoa. Hii itaimarisha thamani ya utoaji wa huduma za afya kwa muda mrefu.
"Nawaomba Madaktari ambao mmepangwa kutoa huduma za ubingwa na bobezi mkawe chachu na hamasa ya kujifunza kwa wataalam mtakaowakuta ili na wao waweze kuwa mabingwa kama nyie kwa kuwashirikisha wakati mkitoa huduma," aliongeza Mpogolo.
Kwa upande wake Mratibu wa zoezi hilo kutoka Wizara ya Afya, Faraja Mgeni ameshukuru Mkoa wa Dar es Salaam kwa mapokezi mazuri.
Amesema hadi sasa, zaidi ya wananchi 154,000 wameshafikiwa na kupata huduma za kibingwa katika wilaya 180 za mikoa mbalimbali nchini.
Aidha wametoa wito kwa wakazi wa jiji na maeneo ya jotani wajitokese kwa wingi kuchangamkia fursa hii ya kipekee ya kupatiwwa matibabu bora na salia salama.




