Breaking News

MHANDISI ROBERT GABRIEL ACHUKUA FOMU YA UBUNGE GEITA MJINI, KUMVAA KANYASU

Geita – Mhandisi Gabriel Luhumbi Robert, Mkuu wa Mkoa mstaafu, ametangaza rasmi nia ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Geita Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), na tayari amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama hicho.

Kwa hatua hiyo, Mhandisi Robert anajitosa kumtoa Mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Constantine Kanyasu, katika kinyang’anyiro cha ndani ya chama kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao. Hatua hii imeibua mvuto mpya wa kisiasa ndani ya CCM Geita, huku wafuasi wa chama wakisubiri kwa hamu mchujo wa wagombea.

Mhandisi Robert anaelezwa kuwa na rekodi ya utumishi wa muda mrefu serikalini, na sasa analenga kuhamishia uzoefu wake kwenye uwakilishi wa wananchi bungeni.