MSAMA ATOA UFAFAMUZI TUHUMA ZA KUFUKUZWA KWENYE NYUMBA YAKE
Dar es salaam - Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama, amewataka Watanzania kupuuza taarifa zinazosambaa mitandaoni zinazodai kuwa amefukuzwa kwenye nyumba yake iliyopo Upanga, Dar es Salaam.
Akizungumza na vyombo vya habari, Msama amesema video zinazosambazwa ni za kupikwa na zinalenga kumchafua hasa katika kipindi hiki cha harakati za kisiasa kuelekea uchaguzi.
"Video zinazosambaa zinatumika na watu wasio na nia njema na mimi, na zina lengo la kunichafua hasa kipindi hiki cha vita za ubunge," alisema Msama.
Msama ameongeza kuwa ataendelea kuchapa kazi kwa bidii na hatatetereka na uzushi unaoenezwa dhidi yake. Ametoa wito kwa wananchi kuzingatia taarifa sahihi na kuepuka kuzua au kusambaza habari za upotoshaji.




