KITUNDU ACHUKUA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA KIVULE KUPITIA CCM
Dar es Salaam – Aliyekuwa Diwani wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tickey Kitundu, amechukua fomu ya kuwania ubunge wa Jimbo la Kivule kwa tiketi ya CCM.
Kitundu alikabidhiwa fomu hiyo Juni 30, 2025, na Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Sylvester Yared, katika ofisi za chama hicho.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Kitundu alieleza dhamira yake ya kushirikiana na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Jimbo la Kivule.
"Nina nia ya dhati kusaidia juhudi za Rais wetu katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa Kivule. Nitajikita katika kutatua kero za wananchi na kuleta mabadiliko chanya," alisema Kitundu.
Mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu za uteuzi ndani ya CCM umeendelea kwa wagombea mbalimbali katika maeneo tofauti nchini, huku ushindani ukiwa mkubwa kwenye baadhi ya majimbo.







