KILOMETA 5,500 ZA MKONGO WA TAIFA ZAJENGWA CHINI YA RAIS SAMIA
Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuimarisha miundombinu ya mawasiliano nchini kupitia upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. Tangu mwaka 2021, mtandao wa mkongo huo umeongezeka kutoka kilomita 8,319 hadi kufikia kilomita 13,820 mwaka 2025.
Ongezeko hilo la kilomita 5,501, sawa na asilimia 66.1, limeongeza uwezo wa kusafirisha data kwa kasi kubwa (high bandwidth), kupunguza gharama za intaneti kwa wananchi na taasisi mbalimbali, pamoja na kuongeza uthabiti wa huduma za mawasiliano nchini.
Hatua hii inalenga kuimarisha uchumi wa kidijitali, kuongeza upatikanaji wa huduma za mawasiliano vijijini na mijini, na kuchochea shughuli za kijamii na kiuchumi zinazotegemea teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA).