Breaking News

AMANI KWANZA: WANANCHI PUUZENI KELELE ZA UCHOCHEZI, MSIRUDIE MAKOSA YA MAJIRANI

Picha na mtandao 

Na Mwandishi wetu - Kuelekea Uchaguzi Mkuu, Watanzania wameonywa kutozisikiliza kelele za watu wasioishi nchini wenye lengo la kuvuruga amani na utulivu wa taifa, huku wakikumbushwa kujifunza kutokana na machafuko yaliyotokea katika mataifa jirani baada ya vurugu za kisiasa.

Wito huu umetolewa Oktoba 24, 2025 katika moja ya kampeni za kuuza sera kwa lengo la kuwania kukamata dola , ambapo viongozi walisisitiza kuwa amani ya Tanzania ndio urithi mkubwa wa taifa, usiopaswa kuchezewa.

Tahadhari Dhidi ya Propaganda za Kigeni

Imesisitizwa kuwa Watanzania hawapaswi kuvurugwa na kelele na propaganda zinazotoka nje ya mipaka ya nchi. Wananchi wametakiwa kuendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo vimejipanga kikamilifu kulinda amani na utulivu wa Taifa kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu.

Amani imeelezwa kuwa ndiyo msingi wa maendeleo na ustawi wa Taifa, kwani bila amani hakuna uwekezaji, elimu, afya, wala ibada zinazoweza kufanyika kwa uhuru.

"Amani inatuwezesha kuabudu kwa uhuru, kufanya kazi, kuzalisha mali, na kuona maendeleo tunayojivunia leo. Tukilinda amani, tunalinda maisha yetu na vizazi vijavyo," ilisisitizwa.

Somo Kutoka kwa Mataifa Jirani Ili kuonyesha umuhimu wa kulinda amani, Watanzania wameonywa kujifunza kutokana na historia ya mataifa jirani yaliyopoteza amani. Mifano ya machafuko hayo ni pamoja na: Kenya (2007): Watu zaidi ya elfu moja walifariki na zaidi ya laki tatu walipoteza makazi kutokana na vurugu za kisiasa. Ivory Coast (2010): Watu mia nne na sitini walipoteza maisha kutokana na machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi.

Imesisitizwa kuwa machafuko haya yameacha somo kubwa kwa Afrika nzima, kwamba amani ni urithi usiopaswa kuchezewa. 

Tanzania itaendelea kuwa kisiwa cha amani na kimbilio la wengi barani Afrika, endapo wananchi wataendelea kushirikiana kudumisha hali ya utulivu na mshikamano.