Breaking News

ATHENA YAAJIRI MBOBEZI KUSUKUMA MBELE UJENZI MIUNDOMBINU YA KIDIJITI AFRIKA MASHARIKI

Na Mwandishi wetu - Athena Core Technologies, kampuni inayojenga miundombinu ya kidijitali Afrika Mashariki, imetangaza kumteua Jorge Rodriguez kuwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wake mpya.

Rodriguez, ameshashika nyadhifa za utendaji katika kampuni ya América Móvil (pamoja na Telmex USA, Claro Enterprise Solutions, na HITSS USA) na hivi karibuni Sorenson Communications.

Uteuzi wa Rodriguez umefanyika wakati Athena ikipanua shughuli zake kwa kuhakikisha uwapo wa jukwaa jumuishi la kidijitali litakalohusisha nyaya za chini ya bahari (subsea capacity), vituo vya data visivyo na upendeleo (carrier-neutral data centers), na mkongo wa kitaifa (nationwide fiber networks). 

Ujenzi wa miundombinu hiyo imekusudiwa kutoa njia mbadala za mawasiliano yenye kasi na ufikiaji wa uhakika wa intaneti katika ukanda wote wa Afrika Mashariki.

Rodriguez mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 30 katika uongozi wa sekta za mawasiliano na teknolojia duniani, akikuza majukwaa makubwa ya mawasiliano katika nchi za Amerika na maeneo mengine, huku akionesha rekodi nzuri ya kuleta mabadiliko chanya ya kiutendaji amesisitiza umuhimu wa jukumu la Athena katika kuunganisha mataifa, kuwezesha ukuaji wa uchumi, na kuunda Afrika inayoongozwa na kipaumbele cha teknolojia ya 'cloud'. 

Uzoefu na dira ya Rodriguez unatazamiwa kuimarisha nafasi ya Athena kama kinara wa soko katika kutoa miundombinu ya kidijitali inayoaminika na yenye ufanisi barani.

Athena Core Technologies imelenga kuziba pengo la kidijitali na kuwawezesha serikali, biashara, na jamii kustawi .