Breaking News

MABASI YA MWENDOKASI YARUSHIWA MAWE, WATATU WAKAMATWA DAR ES SALAAM


Watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa tuhuma za kuhusika na uharibifu wa miundombinu ya mabasi ya mwendokasi.

Watuhumiwa hao walikamatwa usiku wa kuamkia Oktoba 1, katika maeneo ya Gerezani Kariakoo na Magomeni baada ya mabasi na vituo vya mwendokasi kurushiwa mawe na kusababisha vioo kuvunjika.

Kwa sasa mahojiano yanaendelea, huku Polisi wakisema wanasaka watu wengine waliokimbia baada ya tukio hilo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam amewaonya wananchi kuepuka kujihusisha na vitendo vya uharibifu wa mali za umma, akisisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahusika.