Breaking News

TAMWA NA ASASI ZA WANAWAKE WAHIMIZA WANAWAKE KUSHIRIKI KATIKA SIASA NA UPIGAJI KURA OKTOBA 29

Muungano wa Asasi za Wanawake na Watetezi wa Usawa wa Kijinsia Tanzania zinazotetea makundi maalum ikiwamo wanawake, watoto na vijana wanawake, wameungana kwa pamoja kuhimiza umma kuhusu ajenda muhimu ya ushiriki wa wanawake katika siasa na uongozi sambamba na kuhimiza ushiriki wa wanawake katika upigaji kura siku ya Oktoba 29 mwaka huu

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 23,2025 Jijini Dar es Salaam ,Mwanzilishi wa TAMWA,Rose Haji amesema
tunatoa wito kwa vyombo vya habari kutoa nafasi sawa kwa wagombea wanawake kuratibu midahalo,makala na mijadala inayojenga uelewa wa umma juu ya uwezo na mchango wa wanawake katika maendeleo ya Taifa

Tanzania imepata kiongozi mkuu wa nchi mwanamke, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, ambaye pia anawania kiti hicho cha urais kwa tiketi ya CCM na mwaka huu kumekuwa na wagombea wengine wanawake wa urais, akiwemo Saumu Rashid kutoka UDP na Mwajuma Mirambo –UMD.Kwa upande wa wagombea wenza wa urais kutoka vyama vingine ni pamoja na Eveline Wilbard Munis (NCCR), Husna Mohamed Abdallah (CUF), Aziza Haji Selemani (D. MAKINI), Amani Selemani Mzee (TLP), Chausiku Khatibu Mohamed (NLD), Sakia Mussa Debwa (SAU), Chuma Juma Abdallah na Devotha Minja (CHAUMA).Hii ni hatua kubwa ya kidemokrasia kwa Tanzania na kwa ajenda ya ushiriki wa wanawake katika siasa na uongozi.",amesema mwanzilishi Haji

Amesema kwamba ushiriki wa wanawake katika siasa na uongozi ni miongoni mwa vipaumbele vya asasi za kiraia zenye mrengo wa jinsia. Kwa hiyo tunaamini wakiwapo viongozi wanawake, kutakuwa na hatua bymahsusi katika kuongeza kipato na maendeleo ya mwanamke. 

Aidha, amesema kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi chache za Afrika ambazo zimepiga hatua katika ajenda ya ushiriki wa wanawake katika siasa na uongozi

Amesema kwamba ushiriki wa wanawake katika siasa na uongozi ni miongoni mwa vipaumbele vya asasi za kiraia zenye mrengo wa jinsia. Kwa hiyo tunaamini wakiwapo viongozi wanawake, kutakuwa na hatua bymahsusi katika kuongeza kipato na maendeleo ya mwanamke. 

Aidha, amesema kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi chache za Afrika ambazo zimepiga hatua katika ajenda ya ushiriki wa wanawake katika siasa na uongozi.