Breaking News

UDSM: HATUHUSIKI ΝΑ TAMKO LILILOTOLEWA NA UDASA

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimesema hakitambui wala hakihusiki kwa namna yoyote na tamko lililotolewa na Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) Oktoba 23, 2025.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa chuo hicho imesema imesisitiza kuwa UDASA ni Jumuiya ya kitaaluma yenye uongozi na misimamo yake binafsi ambayo haiwakilishi msimamo wa chuo.

"UDSM inaendelea kuwa taasisi ya umma, inayozingatia misingi ya kitaaluma, katiba, sheria za nchi na maadili ya umma, na kujikita katika mijadala yenye tija kwa maendeleo endelevu na mshikamano wa kitaifa," imesema UDSM. 

Aidha, chuo hicho kimetoa wito kwa Watanzania wote wenye sifa za kisheria kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 kwa amani, utulivu na uzalendo.