DKT. MWAINYEKULE ATAJA BEI YA KIKOMO ZA BIDHAA ZA MAFUTA YA PETROL NOVEMBA, ATOA NENO KWA WAUZAJI
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kwa Tanzania Bara zitakazotumika kuanzia leo Novemba 5, 2025.
Bei hizo zimetangazwa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Dk James Mwainyekule ambapo ameweka wazi kuwa bei hizo ni za rejereja na jumla.
Amesema bei kikomo za rejareja kwa lita moja ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa mkoani Dar es Salaam ni shilingi elfu 2,752 kwa petroli, 2,704 diseli na 2,774 mafuta ya taa.
Tanga ni shilingi 2,813, 2,766 na 2,835 na Mtwara 2,844, 2,797 na 2,866.
"Bei kikomo za jumla kwa Dar es Salaam, Petroli ni shilingi 2,612.48, Dizeli 2,564.79 na Mafuta ya Taa 2,634.35, Tanga 2,618.39 na 2,575.81 na Mtwara 2,618.69 na 2,582.27," amesema.
Dk Mwainyekule amewataka wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta ya petroli kwa rejareja na jumla kuuza mafuta kwa bei zilizotangazwa.
Amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yeyote atakayekiuka agizo hilo.




