Breaking News

KATAA UCHOCHEZI: SOMO LA AMANI LINAREJEA TENA TANZANIA

Taifa la Tanzania linaonekana kuibuka na somo kubwa kufuatia kipindi kifupi cha machafuko na vurugu, huku wananchi wengi wakisisitiza tena na tena umuhimu wa amani, mazungumzo, na umoja kama njia pekee ya kusonga mbele. Kauli ya "Kataa Uchochezi" imekuwa wito wa kitaifa baada ya athari za vurugu za hivi karibuni kuonekana wazi.

Kutokana na maoni mengi ya wananchi kwenye majukwaa mbalimbali, kuna hisia kali kwamba Watanzania wamekuja kutambua thamani halisi ya amani baada ya kuipoteza kwa muda mfupi.

"Daaa kweli tumakuja kujua umuhimu wa amani pale tulipoipoteza kwa muda," alisema mmoja wa wananchi Abdallah Mawata akielezea hali hiyo. Mwingine aliongeza kwa msisitizo, "Tumeiona thamani ya amani yetu."

Maoni haya yanawakilisha makubaliano mapana kwamba machafuko na maandamano hayajengi, bali yanarudisha nyuma maendeleo ya taifa na kuvuruga maisha ya kila siku.

Baraka Nyange mwendesha bodaboda alisema kwamba kutulia kwa hali kunafungua milango ya shughuli za kiuchumi, jambo ambalo wananchi wengi wanalikumbatia kwa mikono miwili.

Ingawa wananchi wameanza kufungua tena biashara zao, kuendelea na kazi za mikono, na kurejesha utaratibu wa kulea familia katika hali ya utulivu. bado tegemeo la kutoka kila siku kutafuta kipato cha kesho,limeonesha umuhimu wa amani katika kulea familia.

Wananchi wameonyesha wasiwasi wao juu ya uharibifu wa mali na miundombinu, wakisisitiza kuwa vitendo hivyo "vinakwamisha maendeleo ya nchi yetu" na "vinarudisha nyuma sana uchumi." huku wakisema kwamba hayakuwa maandamano bali uharibifu kwa kuwa maandamano mtu anaeleza asichokipenda lakini si kwa kuifanya uharibifu na kupora.

Ujumbe mkuu unaojitokeza ni wito wa kulinda amani na kukataa vitendo vyovyote vya uchochezi vinavyoweza kuvuruga utulivu wa taifa.

"Watanzania tuliende amani ya nchi yetu tusikubali wapotoshaji wanao chochea kuvuruga amani ya nchi yetu," ni kauli inayotolewa na wengi.

Ujumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) ulisisitiza umuhimu wa mazungumzo, mshikamano, na upendo kama njia bora ya kutatua tofauti.

Taifa sasa linaonekana kusimama kama taifa lililojifunza, likisisitiza kwamba "Amani si udhaifu, ni nguvu inayotuwezesha kusonga mbele," na kwamba Tanzania bila vurugu na maandamano inawezekana.