Breaking News

MCHANGE: HATUWEZI KUUZA UHURU WETU KWA WAZUNGU

Dar es salaam - Mwenyekiti wa Kituo cha Wanahabari Watetezi wa Rasilimali za Taifa (MECIRA), Habibu Mchange, amekemea vikali kauli za baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaodaiwa kutaka kuirudisha Tanzania kwenye mifumo yenye sura ya ukoloni au utumwa.

Amesema hayo leo, Desemba 12, 2025 jijini Dar es Salaam, wakati akijibu hoja zilizotolewa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, kufuatia tamko la chama hicho.

Mchange amesisitiza kuwa MECIRA, kama sehemu ya Watanzania, inawakumbusha wanasiasa wote kwamba maslahi ya Taifa yanapaswa kupewa kipaumbele kuliko maslahi binafsi au ya vyama vyao vya siasa.