AMBONI ADVENTURE RUN, FURSA YA KUTANGAZA MAPANGO YA AMBONI TANGA
Na Kassim Nyaki, Amboni Tanga - Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro imeshiriki na kudhamini mbio za AmbonI Adventure run zilizofanyika leo tarehe 31 Januari 2026 jijini Tanga kwa lengo la kutangaza vivutio vya utalii hususan mapango ya Amboni yanayosimamiwa na Mamlaka yah ifadhi ya Ngorongoro
Mbio hizo za umbali wa kimomita 6, 10 na 20 ambazo zimehudhuriwa na wakimbiaji zaidi ya 500 kutoka maeneo mbalimbali nchini zimeanzia katika viwanja vya Shule ya Sekondari Galanos hadi Mapango ya amboni ambapo washiriki wa mbio hizo wamepata fursa ya kufanya utalii wa ndani katika mapango hayo.
Kaimu meneja uhusiano wa Ngorongoro Hamis Dambaya ambaye ameshiriki mbio hizo kwa kukimbia kilomita 10 ameeleza kuwa Ngorongoro imeamua kuungana na wadau mbalimbali kuendelea kutangaza vivutio vilivyoko katika mapango ya Amboni ili yaendelee kujulikana kitaifa na kimataifa na kuvutia wageni wengi kutembelea na kuona vivutio vinavyopatikana katika mapango hayo na kupataa taarifa mbalimbali ikiwemo historia ya wapigania uhuru.
Msimamizi wa Mapango ya Amboni Afisa Uhifadhi Daraja la kwanza Ramadhan Rashid ameeleza kuwa baadhi ya vivutio vinavyopatikana katika Mapango ya Amboni ni pamoja na maumbo ya asili ya kijiolojia, vivutio vilivyochongwa na maji kama meli, mlima Kilimanjaro, kanisa, msikiti, shughuli za kimila na mataambiko, ndege ndani ya mapango, pango la jinsia, Pango la fatuma ambalo watu hulitumia kuomba mchumba wa kuoa, mimea ya aina mbalimbali, mto pamoja na mazingira asilia yanayopaambwa naa upepo mwanana wa bahari ya hindi.
Mkuugenzi wa Kale Amboni Caves Sophia Mulamula ameeleza kuwa Mbio za Amboni Adventure Run ambazo zimefanyika kwa msimu wa tatu na kuhudhuriwa na wakimbiaji takriban 500 zinatendelea kuboreshwa ili kuvutia wakimbiaji wengi zaidi mwaka ujao 2027
“Tumefanya tathmini kwa miaka hii miwili tumeona mbio hizi zinavutia watu wengi, tunaamini mwakani tunaboresha vitu vingi zaidi ili tupate wakimbiaji wengi kwa lengo la kutangaza vivutio vya utalii, kutangaza nchi yetu lakini kuendelea kuhamasisha utalii wa michezo” alilisitiza Mulamula.









