Breaking News

MGOMBEA WA NLD ACHUKUA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA PERAMIHO

Ruvuma - Mgombea wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Mheshimiwa Mhagama Hamisi Yusufu, amechukua fomu ya kuwania ubunge katika Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo, Mhagama alisema kuwa ameazimia kugombea nafasi hiyo ili kuwatumikia wananchi wa Peramiho, akiahidi kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili, hususan kero ya miundombinu ya barabara.
Mhagama alieleza kuwa endapo wananchi watampa ridhaa ya kumchagua, atahakikisha anasimamia ipasavyo uboreshaji wa barabara ili kurahisisha shughuli za kijamii na kiuchumi katika jimbo hilo.

Mchakato wa uchukuaji wa fomu kwa wagombea unaendelea katika vyama mbalimbali vya siasa kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.