Breaking News

RC CHALAMILA AIPA WIKI MBILI MWENDOKASI KUKAMILISHA UJENZI WA BARABARA YA MWENGE – POSTA

Na Neema Mpaka - Mkuu wa mkoa wa Dare es salaam Albert Chalamila amefanya ziara ya kikazi leo ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa mabasi yaendayo haraka( mwendokasi) katika barabara ya kutoka mwenge mpaka posta.

Katika ziara hiyo mkuu wa mkoa alipokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kutoka kwa mkandarasi na mtaalamu wa ujenzi akitaka kujua hatua iliyofikiwa pamoja changamoto zinazoukabili mradi huo.

Akizungumza na mkandarasi mkuu wa mkoa amesisitiza umuhimu wa kuongeza Kasi ya ujenzi ili kuanza kuwahudumia wananchi wa jiji la dare es salaam.
Aidha amesema kuwa mradi huo ni muhimu katika kupunguza msongamano wa magari na kuboresha huduma ya usafiri kwa wananchi.

"Nakupa wiki mbili uwe umekamilisha ujenzi wa barabara hii, na nitarejea tena kufanya ukaguzi ili kujiridhisha kama maendeleo yanayoonekana katika utekelezaji wa mradi huu" amesema Chalamila.

Aidha mkuu huyo wa mkoa amesisitiza kuwa serkali haitavumilia ucheleweshaji usio na sababu za msingi katika miradi ya maendeleo na inapaswa kutekelezwa kwa ufanisi, ubora na kwa kuzingatia muda uliopangwa.