RC CHALAMILA AKAGUA MRADI WA DARAJA LA MKWAJUNI,AAGIZA UKAMILIKE KWA WAKATI
Na Neema Mpaka - Mkuu wa mkoa wa Dare es salaam Albert Chalamila amefanya ziara ya kikazi leo katika wilaya ya kinondoni kwa lengo la kukagua na kufuatilia maendeleo ya miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika wilaya hiyo.
Katika ziara hiyo mkuu wa mkoa alikagua mradi wa ujenzi wa daraja la mkwajuni ambapo alipata maelezo kutoka kwa wataalamu juu ya hatua iliyofikiwa na changamoto zilizopo katika utekelezaji wa mradi huo.
Aidha mkuu wa mkoa baadaya ya kupokea maelezo hayo amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyokidhi ubora unaotakiwa ili kuwanufaisha wananchi.
"Miundombinu bora ya barabara na madaraja ni chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii" amesema Chalamila.
Aidha amesema kwa watumiaji wa barabara wanapaswa kutumia barabara hizo vizuri bila kuharibu miundombinu iliyopo na kuzilinda ili zidumu kwa muda mrefu.
Kadhalika amewataka wakandarasi kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi wakizingatia ubora na usalama , pamoja na kushirikiana na wananchi ili kuhakikisha miradi hiyo inaleta tija kwa jamii ya kinondoni na mkoa wa Dare es salaam kwa ujumla.








