RC CHALAMILA AWASIHI WAKAZI WA DAR KUIMARISHA UMOJA NA MSHIKAMANO
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Chalamila amewataka wakazi wa Dar es Salaam kuendeleza umoja na upendo miongoni mwao, akisistiza kuwa mwezi mtukufu wa Ramadhani ni fursa ya kuimarisha mshikamano wa kijamii na kusaidiana.
Akizungumza katika hafla ya Iftar maalum kwa wakazi wa Mkoa huo mapena leo Februari 27, 2026 ambayo imefanyika katika ukimbi wa Diamond Jubilee, RC CHALAMILA amesema Serikali ya Mkoa itaendelea kushirikiana na Viongozi wa Dini katika kudumisha amani na utulivu.
"Nitoe rai kwa wakazi wa Dar es Salaam kuendeleza umoja na upendo miongoni mwetu, katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani ni fursa ya kuimarisha mshikamano wa kijamii na kusaidiana." Alisema Rc Chalamila.
Alisema Serikali ya Mkoa itaendelea kushirikiana na Viongozi wabalimbali wa Dini katika kudumisha amani na utulivu.
Kwa upande wa Mufti Mkuu wa Tanzania, Dkt Abubakar Zubeir bin Ally ameipongeza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kuandaa Iftar hiyo, akieleza kuwa matukio ya aina hiyo huimarisha uhusiano kati ya Serikali na Jamii ambapo ametoa wito kwa watanzania kuendelea kuiombea nchi na kuzingatia maadili katika kipindi hiki cha Ramadhani.
katika Hafla hiyo ambayo hudhuriwa viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali pamoja na wananchi kutoka maeneo tofauti ya Jiji la Dar es Salaam ilihitimishwa kwa futari ya pamoja iliyoambatana na mawaidha mafupi ya kidini huku washiriki wakionyesha furaha na mshikamano mkubwa





.jpg)






