Breaking News

RC CHALAMILA AKABIDHI ZAWADI ZA EID KWA WILAYA 5 DSM

# Asema zawadi hizo ni mkono wa Eid kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt Samia.

Na mwandishi wetu - Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amekabidhi zawadi mbalimbali ikiwemo mchele, mafuta ya kupikia, sabuni na tende ambazo zimetolewa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya makundi ya watu wenye uhitaji Mkoani humo katika kusherehekea sikukuu ya Eid Alfitri ambayo husherehekewa baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza wakati akikabidhi zawadi hizo kwa wakuu wa wilaya tano za Mkoa huo RC Chalamila amesema huo ni utamaduni wa Rais kila mwaka ambapo kwa mwaka huu ametoa Mchele tani moja kwa kila Wilaya, viroba 30 vya sukari vyenye uzito wa kilo 20 kila kimoja, dumu 10 za mafuta ya kula, mbuzi sita, Sabuni viroba 10 na tende boksi tatu kwa kila wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam.
Aidha RC Chalamila amesema Rais ameonesha mfano wa kutoa zawadi kwa familia zenye uhitaji kama kielelezo chema ili viongozi wenge waweze kuunga mkono juhudi hizo na hatimaye makumdi yote ya wenye uhitaji yafikiwe

Mara baada ya Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila kukabidhi zawadi hizo kwa wakuu wa Wilaya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amefanya utelelezaji wa kufikisha misaada hiyo kwa wahitaji wilayani humo ambapo amekabidhi mkono huo wa Eid kwenye takriban vituo 7 vyenye watu wenye uhitaji ikiwemo kituo cha Ashura Foundation kilichopo vimgunguti pia wakuu wengine wa Wilaya wameendelea kutoa zawadi hizo katika maeneo yao.
Kwa upande wake Afisa ustawi kutoka kituo cha kulea watoto wenye uhitaji cha Ashura Foundation kilichopo vingunguti Waziri Saidi ameeleza furaha yake baada ya kupokea mkono huo wa Eid ambapo amemshukiru Rais Dkt Samia kwa kuwakumbuka.